SARAH K LISEME SONG

Tuesday, April 10, 2012

STEVEN KANUMBA AANDIKA HISTORIA NYINGINE BAADA YA BABA WA TAIFA

Watanzania hii leo wameweza kumuaga kwa heshima mwigizaji nyota marehemu Steven Kanumba katika ibada iliyofanyika kwenye viwanja vya Leaders club Kinondoni jijini Dar es salaam,na kuhudhuriwa na Makamu waRais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mh.Dkt Gharib Bilal,mke wa Rais mama Salma Kikwete na viongozi wengine pamoja na familia ya marehemu,waigizaji wenzake pamoja na wanakwaya wa kwaya ya Neema gospel (NGC)kutoka AIC Chang'ombe alikokuwa muumini na mwanakwaya wa kwaya hiyo.

Umati mkubwa ambao ulikusanyika katika eneo la Leaders club kisha makaburi ya Kinondoni umeweka historia kwajinsi msanii huyo alivyokubalika katika jamii ya Watanzania,mpaka sasa akiwa ameshika nafasi ya pili kupata watu wengi,nafasi ya kwanza ikiwa ni msiba wa Baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye mwili wake ulitolewa heshima za mwisho kwenye uwanja wa zamani wa Taifa jijini Dar es salaam.
Sehemu ambayo ilikuwa ikiandaliwa kuwekwa jeneza lenye mwili wa Kanumba.

Hemed pamoja na Yusuph ambao ni waigizaji wakiingia Leaders asubuhi ya leo kumuaga mwenzao.

Watoto ambao waliigiza na Kanumba wakiwa wanaingia viwanjani hapo asubuhi ya leo.

Mama wa marehemu Steven Kanumba akiwapungia maelfu ya watu asubuhi ya leo kuonyesha shukrani kwa kujitokeza kumuaga mwanae.


Viongozi wa serikali wakiwa wamekaa kwenye jukwaa maalumu.


Kijana Samuel Limbu akiwaongoza wenzake wa Neema gospel Choir kuimba viwanja vya Leaders club.

Wasanii wakiliingiza jeneza la mwenzao viwanja vya Leaders Kinondoni.

Wasanii wakipeleka jukwaani jeneza lenye mwili wa Steven Kanumba.

Waigizaji wakishusha jeneza la mwenzao taratibu jukwaani.

Jukwaa kuu kwaya ya Neema Gospel Chang'ombe wakiimba kumsindikiza mwimbaji mwenzao.


Kuna watu walishindwa kuhimili hisia zao kwa marehemu nakujikuta wakizimia,msalaba mwekundu wakitoa huduma.

Makamu wa Rais Dkt.Gharib Bilal akitoa heshima zake za mwisho.

Mke wa Rais mama Salma Kikwete akitoa heshima zake za mwisho.


Baadhi ya umati wa watu uliokuwepo asubuhi ya leo viwanja vya Leaders club Kinondoni.

Mh.Bernard Membe akitoa heshima zake za mwisho.

Kamanda wa polis mkoa wa Dar es salaam Kova akitoa heshima zake za mwisho.

Wanahabari wakihakikisha hawapitwi na jambo.
KUTOKA MAKABURI YA KINONDONI NAKO HUKO MAELFU YA WATU WALIKUSANYIKA ILI KUSHUHUDIA MAZISHI YAKE,AMBAPO POLISI WALIKUWA NA KAZI YA ZIADA KATIKA ULINZI,AMBAPO PIA TAARIFA ZINASEMA KUNA WATU WAMEJERUHIWA BAADA YA KUANGUKA KUFUATIA TAWI WALILOKALIA KUKATIKA.

1 comment:

  1. Siku zote nikiona picha hii hua napata uchungu san, kwakua Steven Ch KANUMBA alikua msada kwangu. yeye ndie mtu wakwanza alie nifunza hatua zangu zakwanza kwenye kundi la sanaa Great Lakes jijini Bujumbura mwaka 2010 kipindi alikuja kupiga show pamoja nadada IRENE Uwoya.MUNGU ailaze roho ya marehemu mahali pema.KANUMBA The great sito kusahau kwawema ulionitendea

    ReplyDelete