SARAH K LISEME SONG

WANAMEREMETA

WANAPENDEZA
 
 


MAIMATHA AFUNGA PINGU ZA MAISHA
Mtangazaji maarufu wa TBC television ya taifa Maimatha wa Jesse juzi alifunga pingu za maisha na kutoka katika chama cha ukapera na kuingia katika maisha ya ndoa sherehe iliofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee Vip, Tunawatakia maisha mema katika maisha yenu mapya muwe wavumilivu katika shida na raha katika kuijenga familia yenu Mungu yuko nyuma yenu katika ndoa yenu hivyo msimuweke kando siku zenu zote za maisha yenu


Wageni waalikwa wakifuatilia jambo lililokuwalikiendelea siku hiyo iliojaa mastaa kibao wa nchini Tanzania

Flowerrrrrrrrs

Wakati wa burudani ulifika na mwanamuziki wa taarabu Dada yetu Hadija 
Kopa alitumbuiza katika harusi na kuleta burudani ya aina yake


Penny na Kajala Masanja kulia 

Penny


Kajala

Sajenti

Wamependeza jamani

Mainda

Hadija Kopa akifanya mambo yake

Kama kawaida ya madada zetu bize na simu 

Picha ya kumbukumbu

Pamoja tunawakilisha

-----------------------------------


CHRISTINA MAANDE WA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI B AVISHWA PETE YA UCHUMBA 
Christina akionekana mnyenyekevu mbele ya kanisa na mbele ya Mchungaji wa kanisa hilo, Dkt Getrude Rwakatare baada ya kuvishwa pete na mchumba wake Jese.  Dada huyu alionekana kutoa machozi kama ishara ya furaha kwa kitendo cha kupata mchumba mwenye msimamo. 

Waumini walionekana kuguswa sana na tendo hilo, watu walicheza na kutoa zawadi  za kumpongeza. Mama Getrude Rwakatare alionekana ni mtu aliyeguswa sana na kilio cha furaha cha Christina na hasa pale alipomvisha kitenge mchungaji wake kama ishara ya upendo.

Na sasa tuone yaliyoajili

Jese (kulia) akimsubiri mchumba wake Christina madhabahuni

 Wapambe wa Bwana harusi mtarajiwa, Jese wakijiaandaa  kupongeza

 Wachungaji wa Mlima wa Moto Mikocheni B wakishuhudia shughuli nzima ya madhabahuni.
Kuanzia kulia ni Mama Lucas, Mch. Kyando, Mchungaji ambaye jina lake halikupatikana, Mchungaji Lukumai
 Bibi harusi mtarajiwa, Christina aliyevalia orange akiwa madhabahuni na mchumba wake aliyepigilia suti kali.
 Haya haya siku imewadia..Christina akiwa amepiga magoti huku akivishwa pete na mchumba wake  Jese Onesmo , madhabahuni
 Jese Onesmo akimshikilia kwa makini mchumba wake
 Kilichofuata ni maombi makali kutoka kwa wachungaji
 Mchungaji msaidizi, Lukumai (kulia) na Mchungaji Getrude Rwakatare akiwaombea wachumba hao

 Mama nikupe nini.......nimempata mchumba wangu mzuri.....kilio cha furaha mbele ya mchungaji wake.
 Mchungaji Getrude Rwakatare akifurahia zawadi ya kitenge kutoka kwa Christina
 Haya sasa...wapambe kuvamia madhabahu kumpokea Bwana Harusi mtarajiwa
 Mwimbaji mwalikwa akimwimbia Bwana wimbo wa Ebeneza
 Kilio cha furaha kilitawala kwa wachumba hawa
Maombi yakiendelea