SARAH K LISEME SONG

Wednesday, July 25, 2012

NDOA YA MWIGIZAJI WA FILAMU ZA KIBONGO DOTNATA YAVUNJIKA


BAADA ya staa wa kitambo katika filamu, Husna Poshi ‘Dotnata’ (pichani) kurudi  katika dini yake ya Kikristo huku akiwa na ndoa ya Kiislamu na mumewe Mohammed Poshi, Sheikh Mohammed Ramadhan wa Msikiti wa Kichangani, Magomeni jijini Dar amesema ndoa ya wawili hao imevunjika.
Akizungumza na Tollywood Newz, jijini Dar es salaam, Sheikh Mohammed alisema kwa sheria ya Kiislam, wawili hao hawana ndoa bali watakuwa wanafanya zinaa.
“Dotnata atakuwa anamtania Mungu kwa kufanya mchezo wa kuzihama dini, lakini namtaka aache kumpikia futari Poshi na hata kama watakuwa wakifanya tendo la ndoa basi wajue  wanachokifanya ni uzinifu tu,” alisema Sheik Mohammed.
Hivi karibuni, Dotnata kupitia  gazeti la Ijumaa alisema kuwa ameamua kurudi katika ukristo na hana tatizo na mumewe kwani wanaendelea kama kawaida.

No comments:

Post a Comment