SARAH K LISEME SONG

Religious News


WAZIRI MKUU MSTAAFU LOWASA USO KWA USO NA TB JOSHUA-NIGERIA

BAADA ya kuandamwa na ‘kashikashi’ za kisiasa kwa muda mrefu, Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa (CCM), ameonekana ‘laivu’ runingani akifuatilia kwa karibu ibada ya Kiongozi Mkuu wa Huduma ya Kikristo ya Synagogue Church of All Nations (SCOAN), Mtume na Nabii Temitope Balogun Joshua ‘T.B Joshua’ huko Lagos, Nigeria.
Ishu hiyo ambayo imekuwa gumzo katika mitandao fulani fulani ilijiri hivi karibuni ambapo waziri mkuu huyo mstaafu alionekana kupitia Runinga ya Emmanuel TV.

Katika ibada hiyo iliyokuwa na ‘taito’ ya Sunday Live Service, ujumbe wa siku hiyo ulikuwa ni kushinda woga katika kujaribu kutenda jambo lolote.
T.B Joshua ni mmoja wa viongozi wenye heshima duniani aliyejipatia umaarufu kutokana na unabii anaoutoa kuhusu masuala mbalimbali, uponyaji kwa njia ya maombi na maombezi ya kawaida.



-------------------------------------------


KISA CHA KWAYA YA CHRIST AMBASSODORS, RWANDA 


Hichi ndiyo kilichoipata Kwaya ya Ukweli Christ Ambassadors Kutoka kule nchini Rwanda. 

Kundi la Ambasadors of christ choir Rwanda kabla ya ajali 

Ambassadors of Christ Choir ni kwaya ambayo kwa sasa inafanya Vizuri sana na nyimbo zake zimekuwa Gumzo hapa nchini. Kundi hili lenye maskani yake nchini Rwanda katika jiji la Kigali hivi sasa limetimiza miezi takribani miwili tangu baadhi ya wanakikundi hicho kufariki dunia tarehe 9/05/2011 walipokuja nchini kwa mualiko wa kwaya ya Acasia Mwenge SDA ya jijini Da es salaam. 

Baada ya kupata Mualiko huo, tarehe 5/05/2011 Kundi hilo lilianza safari ya kuja jijini Dar es salaam kwa ajili ya Uzinduzi wa DVD ya kwaya ya Acasia ambao ulipangwa kufanyika katika ukumbi wa PTA ulio katika viwanja vya Sabasaba jijini Dr es salaam. 

Ambassadors of Christ walifanikiwa kufika Dar es salaam tarehe 6/05/2011. Kundi hili liliweza kushiriki ibada ya sabato siku ya jumamsi ya tarehe 7/5/2011 na lilialikwa katika Interview katika kituo cha Redio cha Morning Star Adventist Radio of Tanzania kilichoko jijini Dar-es salaam kwenye kipindi kiitwacho “LULU ZA INJILI” ambacho hungozwa na Bro Emmanuel Maduhu. 

Wakiwa Redioni hapo, kundi hili lilivutia wasikilizaji wengi hasa kwa uwezo wao wa kuimba Live. Tarehe 8/05/2011 ndio siku iliyokuwa ikisubiriwa kwani ilikuwa siku Maalumu kwa kwaya ya Acasia Mwenge SDA Kufanya uzinduzi wa dvd yao ya Pili iitwayo “MNAZARAYO” katika ukumbi wa PTA. 

Kundi hilo likiimba wakati wa uzinduzi wa dvd ya acasia choir katika ukumbi wa PTA jijini Dar es salaam 

Watu kutoka kona tofauti tofauti za jijini Dar walifurika kutaka kuwaona vijana hawa Live wakiwa jukwaani wakimtukuza Mungu. Muda uliwadia na ndipo vikundi mbalimbali vya injili vilitangulia kuimba wakiwemo Voice of Victory wakifuatiwa na Triumph Generation pamoja na Harvesters vyote vya jijini Dar es salaam. 

Muda uliwadia ambapo ukumbi mzima ulizizima kwa furaha na vifijo pindi Ambassadors of Christ walipotajwa kuwa ndio wanafuata kupanda jukwaani. Taratibu huku ala ya nyimbo yao maarufu iitwayo Twapaona vijana hawa walipanda jukwani na ukumbi mzima ulizidi kupiga kelele za furaha. 

Miongoni mwa nyimbo ambazo Ambassadors of Christ walizimba Live siku hiyo ni pamoja na Kazi Tufanye, Yesu Ndiye Njia, Twapaona, Kuna Siku, Huyo ni Yesu, pamoja na nyimbo yao maarufu iitwayo Kwetu Pazuri. Watu wote waliofika ukumbini hapo walibarikiwa na kazi za kundi hili kwa utukufu wa Mungu. 

Kuhusu Ajali 

Baada ya kumaliza huduma tarehe 8/05/2011, kundi zima la Ambassadors of Christ lilianza safari ya kurudi Kigali asubuhi ya tarehe 9/05/2011 kwa njia ya basi. Walipofika Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga mnamo saa tatu usiku walikutana na lori likiwa limepaki barabarani likiwa halina reflector yeyote. Dreva wa gari la kundi hilo hakuweza kulina lorry hilo na pindi alipoliona na kutaka kuliovatake ndipo lori lingine lilikuwa likija kwa kasi hivyo wakakutana uso kwa uso na ajali ikatokea. 






Hali ya Gari la kundi hilo baada ya ajali

Baada ya ajali hiyo iliyotokea kilometa kadhaa kabla ya kufika Rwanda, wanakwaya watatu wa kundi hil Filbert Manzi, Gatare Ephraim pamoja na mtanzania Amos Fares ambaye nayee ni muimbaji wakundi hilo aliyekuwa mbele akielekeza njia walifariki papo hapo. 








Muda mfupi baada ya ajali hiyo kutokea serikali ya Rwanda ilituma Helkopta ya Jeshi la ulinzi la nchi hiyo [RDF] pamoja na Ambulance mbili kwa ajili ya kusafirishia wagonjwa kutoka Kahama kwenda Hospitali ya Mkoa wa shinyanga. Baada ya kufika Hospitali ya shinyanga wahanga hao waliweza kupata huduma ya kwanza na hatimaye walikimbizwa nchini Rwanda katika Hospitali iitwayo King Faisal kwa matibanu zaidi. 

Helkopta ya Jeshi la ulinzi la Rwanda iliyofika kwenye eneo la ajali 

Kwa msaada wa Mungu majeruhi wane wa ajali hiyo walipata nafuu na hatimaye kurutuhusiwa kutoka Hospitali. Taratibu za mazishi zilifanywa ambapo Marehemu Filbert Manzi aliyekuwa mmoja wa vingozi wa kwaya hiy na pia mtangazaji wa kitu kimoja cha Redio nchini Rwanda, pamoja na Gatare Efraimu ambaye alikuwa ni muanzilishi na kiongozi wa kwaya hiyo wa walizikiwa nchini Rwanda, wakati Mtanzania Amos Fares yeye alizikiwa nyumbani kwao mkoani Kigoma. 

Zifuatazo ni baadhi ya matukio ya kundi hilo wakati wakiimba jijini Dar na baada ya ajali hiyo. Majeruhi 

Pichani ni kijana Marc Ndizaye kabla na baada ya ajali ila yeye aliruhusiwa baada ya matibabu. 

Baadhi ya Majeruhi kabla na baada ya ajali 

Waliotangulia 


Hawa ndio watumishi waliopoteza maisha kufuatia ajali hiyo 

Hili ndio kava la Album yao ambapo kushoto mstari wa juu vijana hao watatu Ephraim, Filbert, na Mtanzania Amos hawako nasi tena