SARAH K LISEME SONG

Thursday, October 18, 2012

JENNIFER KYAKA (ODAMA) KUSHUKA NA VIFAA VIPYA VYA MOVIE

 Mmeona mambo haya!!!
 Kazi imepamba moto katika kuchagua stand maridadi kwaajili ya camera
 Duh hii kiboko!!!
 Mama yangu kazi imeanza..ni balaaaa!!!!

 Mhh!! Baada ya kuchagua saaaaana , nikaamua kupumzisha akili kwanza...!!!
 Duh hizi silaha au stand????

 Kazi imeanza sasa kutafuta Boom Mic ya ukweli, si unajua mambo ya sauti kwenye movieeeeee!!!
 Nikikagua Stick ya Boom

 Mhh!! Kazi ipo!!!
 Bei gani kwani??
 Iko poa!!!

 What?

SIKU YA PILI KAZI ILIENDELEA YA KUTAFUTA VIFAA  VINGINE BORA VYA MOVIE.

 Leo kazi ipo!!!
Baada ya zoezi zima kumalizika ukafika wakati wa kupata snaps za kumbukumbu


Wednesday, August 1, 2012

WAKATI MUMEWE PAKISTAN JELA,JACK PATRICK AVUA PETE YA NDOA


Jacqueline Patrick ‘Jack’.

NDOA ya mwanamitindo Jacqueline Patrick ‘Jack’ na mumewe Abdulatifu Fundikira a.k.a Tiff ipo hatarini kuvunjika na habari kutoka jikoni ni kwamba, sasa Jack amevua pete ya ndoa na kubaki na ile ya uchumba.
Jack amefanya kitendo hicho, wakati mumewe akila msoto nyuma ya nondo katika Gereza la Keko, Dar akisubiri kesi yake ya madai ya kujihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya inayoendelea katika Mahakama ya Kisutu jijini.
Mwandishi wetu alimnasa mwanamitindo huyo mrembo, juzikati, jijini Dar es Salaam, akijivinjari bila pete ya ndoa, ndipo alipomuuliza na kumpa majibu ya kushangaza kama siyo ya kushtusha.
SIKIA SABABU ZAKE
“Najua wengi wanaweza kunishangaa wakiniona sina pete yangu ya ndoa, lakini nataka kusema kwamba nipo sahihi na ninajua ninachokifanya. Kwa sasa ni kama sina ndoa au ndoa ipo nusu nusu.
“Siyo makosa nikisema kuwa, naona kama niko mguu ndani mguu nje. Hiyo ndiyo sababu kubwa iliyonifanya niamue kuvua pete yangu ya ndoa,” alisema Jack na kuongeza:
“Unajua mume wangu yupo kwenye matatizo sasa hivi (gerezani) na sijui nini cha kufanya. Kifupi nipo katika wakati mgumu sana, ndiyo maana nimefikia uamuzi wa kuondoa pete kidoleni mwangu.
“Nahisi kama inazidi kuniongezea machungu moyoni mwangu. Sioni faida ya kuivaa kabisa. Afadhali nibaki na hii ya uchumba.”
PEKUPEKU MITAANI

Chanzo chetu makini, kwa sharti la kutotajwa jina lake, kilitupenyezea habari kwamba, tangu Tiff apelekwe mahabusu katika Gereza la Keko, uhusiano kati ya wawili hao umelegalega.
“Kwanza Jack hajaenda kumuona mumewe hata siku moja...unajua hawa bwana, ugomvi wao haukuanza juzi, ni kabla jamaa yake hajapata matatizo. Sidhani kama kuna ndoa tena pale...na hivi mumewe yupo sero ndiyo kabisa,” kilipasha chanzo chetu.
Kikaongeza: “Jaribuni kufuatilia zaidi, lakini wale kuendelea tena, sidhani kama itawezekana kwa hali waliyofikia.”
SAUTI YA FUNDIKIRA KUTOKA KEKO
Tulifunga safari hadi katika Gereza la Keko, Dar kwa lengo la kumtembelea Abdulatifu ikiwa ni pamoja na kufuatilia habari hii.
Huyu hapa anazungumza: “Mke wangu hajafanya kitu kizuri. Inaniuma sana kusikia kwamba amevua pete ya ndoa. Jambo hilo linaninyima amani sana. Mimi kupata matatizo siyo sababu ya msingi ya yeye kuvua pete. Kwa kweli imeniuma sana.”

Monday, July 30, 2012

MUME WA JACK ALILIA NDOA GEREZANI


MUME wa modo Jacqueline Patrick aliyepo nyuma ya nondo za Mahabusu ya Gereza la Keko, Dar es Salaam kwa tuhuma za kusafirisha mihadarati, Abdullatif Fundikira ‘Tiff’ ameililia ndoa yake akisema kuwa amegundua kuna watu wanataka kuivunja kwa makusudi.
Akizungumza tulipomtembelea gerezani hapo wikiendi iliyopita, Tiff alisema kuwa anashangazwa na watu ambao anawaheshimu kuwa ni shemeji zake na ni marafiki wa mkewe lakini wamekuwa wakipepeta umbeya juu ya ndoa yake ili tu ivunjike.
“Aisee inauma sana, lakini Jack hasisikilize maneno ya watu. Akumbuke tumetoka mbali na enzi ya kula bata kwani mimi nikikumbuka kuna wakati natokwa machozi na ukweli ni kwamba siwezi kukubali ndoa yangu ivunjike,” alisema Tiff.

AUNTY EZEKIEL KUFUNGA NDOA MWEZI OCTOBERILE kasumba kwamba hakuna msanii wa bongo muvi anayeweza kuolewa na kudumu ndani ya ndoa, inatarajia kufutwa na msanii Aunty Ezekiel, ambaye anatarajia kufunga ndoa mwezi October mwaka huu, na mpenzi wake anayeishi Dubai ambako ndiko atakoenda kuishi baada ya kufunga ndoa.

Mtandao
, ulifanya mazungumzo mafupi na msanii huyo juu ya maisha yake na filamu kwa ujumla ambapo, alisema kuwa ameamua kuchukua maamuzi hayo ya kutaka kufunga ndoa kwani anahitaji kuishi na mtu ambaye wataweza kupanga naye maisha.

Alidai kuwa mpenzi wake huyo ni Mtanzania ingawa anaishi nje, ambapo anaamini baada ya kufunga ndoa na yeye anataweza kwenda kufanya kazi huko.


“Nilikuwa kimya juu ishu hii lakini nachotaka kusema ni kwamba mambo yangu sasa yameanza na nimeamua kufunga ndoa, hivyo mashabiki wangu nahitaji nao waweze kujua kuwa sasa nimeamua kuchukua maamuzi hayo,”
alisema.

Ezekiel alisema kuwa vikao vya harusi na kupanga itakavyokuwa wameshaaza kukaa, kwani wameanza Jumapili.


Aliongeza kuwa mbali na mchakato huo mkubwa pia mwaka huu wa 2012 kampuni yake inatarajia kufunga mwaka kwa kutoa filamu mbili ambazo anaamini zitakuwa moto wa kuotea mbali.

Saturday, July 28, 2012

RAY AWAPA KWELI MA-MISS WANAOKIMBILIA KWENYE TASNIA YA UIGIZAJI

IDADI kubwa ya warembo wanaofanya filamu ndani ya bongo ni wale waliopita katika mashindano ya ulimbwende iwe wa vitongoji au Taifa, ambapo msanii nguli ndani ya tasnia hiyo Vicent Kigosi ‘Ray’, ametoa somo kwa warembo wengine kuwa wasifikilie tasnia hiyo ni kimbilio lao baada ya kutoka kwenye mashindano yao.


Ray alikaririwa na mwandishi wa DarTalk, akidai kuwa anaamini Tanzania inaweza kupata wanamitindo wazuri lakini anashindwa kuelewa ni kwanini wengi wanakimbilia kufanya filamu baada ya kutoka kwenye mashindano ya U-miss.

Alidai kuwa inawezekana tasnia hiyo ya filamu haina thamani kwani kila mrembo aliyepitia mashindano ya U-miss, baada ya kutoka huko basi anaingia kwenye filamu na kuachana na fani yake ambayo wenda ingeweza kuwa ndio fani yake.

Aliongeza kuwa kila mrembo anayeingia kwenye filamu anadai kuwa fani hiyo ya uigizaji ipo ndani ya damu, hapo ndipo anaposhindwa
kuelewa kwamba kama filamu ni fani inakuwaje aliingia kwenye kwenye ulimbwende on the first place.

“Nawaomba tu warembo wanaotokea kwenye fani hiyo, kama kweli wanahitaji kuliwakilisha vyema taifa letu basi wakaze buti kwenye fani hiyo kwani ni kitu cha aibu sana wanaposhindwa huko na kuja huku kwenye filamu, wanakosa muelekeo”. alisema

Ishu hiyo ndiyo inayofanya hadi tasnia ya filamu Tanzania ishindwe kupiga hatua kwani matatizo kibao yanayotokea ndani ya tasnia hiyo yanasababishwa na wasanii waliotokea kwenye U-miss.

Friday, July 27, 2012

NIMETEMBEA NA WANAWAKE 32 MASTAA-HEMED WA BONGO MOVIE

Source: Bongo flava tz
Kwanza kwa kuanza ningependa kumshukuru Hemed suleiman kwa kuwa mmoja kati ya wavaaji wazuri wa Single buttons ninazozitengeza... picha zote unaziona ni amevalishwa na Martin kadinda..... turudi katika swala zima ambalo limenifanya kuandika Post hii.... Nilitaka kujua ni vijana wangapi watuamiji wazuri wa condoms hasa kwa vijana maarufu. Mtu wangu wa kwanza amekuwa Hemed Suleiman aliniambia: "we jamaa maswali gani hayo bana? mimi kondomu za nini? muda wote mimi nakwenda dry... anakaongezea kuwa alikuwa katika mahusiano na msichana mmoja ambaye hajataka kumtaja na anasema kwa sasa wameachana imepita miezi 3... anasema aliwa kupima nae virusi vya ukimwi na walipojikuta wako safi wakaamua kujilipua kavu kavu....

Alinichosha na majibu yake ikanibidi nihamie katika swali la pili: ambapo nilimuuliza kama amewahi kuwa katika mahusiano na wasichana wa Kitanzania maarufu?


SINA LA KUONGEZA HAPO.HEMED: Marti Martin...... unauliza kengele kanisani??? unadhani kwanini naitwa Hemed PHD? nina taaluma ya kucheza na mioyo ya mabinti hawa wakibongo.... ila tatizo hawanivutii huwa napita tu kwakuwa nina hamu na wakati huo au ninakuwa sipo katika mahusiano na mtu yoyote....

MIMI: Duuh kwahiyo ushampitia nani hii..........?? na nanihiiii........??
HEMED: hilo sio swali... mpaka sasa nishawapitia 32... kwahiyo kuhusu majina katafute mwenyewe huko mtaani mbona stori zipo??


Thursday, July 26, 2012

MWEZI MTUKUFU WAMTEGA NISHA


Salma Jabu ‘Nisha’.

MSANII kunako anga la sinema za Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ ameweka ‘plain’ kuwa yupo katika wakati mgumu kwani Mwezi Mtukufu wa Ramadhan umemtega kwa vile mapenzi yake na jamaa anayedaiwa kuwa ni mume wa mtu ndiyo kwanza yameanza.
Akijilipua kwa Motomoto Newz, Nisha alisema katika kipindi hiki cha swaumu analazimika kukaa mbali na mwanaume huyo kwa sababu si wanandoa.
“Huu ni mtihani jamani lakini sina jinsi, acha nifunge nisije nikaharibu swaumu yangu bure, ila nitamshauri tukimaliza mfungo anioe kabisa,” alisema Nisha.

Wednesday, July 25, 2012

SAJUKI APATA GONJWA BAYA LAMSHAMBULIA UTI WA MGONGO


 
Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’.
 
Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’ akiwa na mkewe Wastara.

PAMOJA na kwamba afya ya staa wa filamu Bongo, Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’ inaendelea vizuri, imegundulika kuwa ana ugonjwa mwingine tofauti na ule uliompeleka India kufanyiwa upasuaji,
Hivi karibuni, Sajuki alirejea kutoka nchini India alipokwenda kwa ajili ya matibabu ambapo alionekana kuwa na mabadiliko makubwa kiafya jambo lililowapa matumaini mashabiki wake.

HABARI MEZANI
Akizungumza na waandishi wetu, juzi, Jumapili nyumbani kwake, Tabata jijini Dar es Salaam, mke wa Sajuki, Wastara Juma alisema mumewe amegundulika kuwa na tatizo lingine walipokuwa nchini India kwa matibabu.
Alisema, hawakutaka kuweka hali hiyo mapema kwa Watanzania kwa kuhofia kusababisha simanzi, lakini sasa wanalazimika kufanya hivyo ili kuwafanya wajue kinachoendelea kwa staa wao.
“Kwa kweli mume wangu bado anaumwa na amegundulika kuwa na tatizo lingine ila tunamshukuru Mungu anaendelea vizuri,” alisema Wastara kwa huzuni nyingi.

NI UGONJWA GANI?
Kwa mujibu wa Wastara, walipokuwa India (katika Hospitali ya Apollo), Sajuki alifanyiwa vipimo mbalimbali ili kubaini matatizo yanayomsumbua ambapo aligundulika kuwa na tatizo kwenye uti wa mgongo na ngozi ya mwili mzima.
“Ana tatizo kwenye mfupa wa uti wa mgongo, lakini pia anasumbuliwa na tatizo jingine kwenye ngozi. Baada ya madaktari kugundua magonjwa hayo walimuanzishia dawa ya kutibu mgongo na mazoezi kwa ajili ya kumuweka sawa.
“Hizo dawa alianza kuzitumia tulipokuja huku, ambapo pia anaendelea na mazoezi. Tatizo lingine ni hilo la ngozi, ambalo pia anaendelea kutumia dawa,” alisema.

KWA NINI MGONGO?
Akifafanua kuhusu ugonjwa unaoshambulia sehemu ya mfupa wa uti wa mgongo, Wastara alisema madaktari walisema, tatizo hilo linasababishwa na kukaa kwa muda mrefu.
“Jambo hilo tulikubaliana nalo, kwa sababu ni kweli Sajuki huwa anakaa muda mrefu kwenye kompyuta kwa ajili ya kazi zake, lakini pia huwa anaendesha gari kwa muda mrefu. Tunaamini ndiyo chanzo cha ugonjwa huo kama madaktari walivyosema,” alisema na kuongeza:
“Lakini baada ya kupata dawa na ushauri  sasa anaendelea vizuri,  kwa sababu pia anafuata masharti aliyopewa vizuri. Huwa nahakikisha anapata muda mrefu wa kupumzika, hakai muda mwingi na haendeshi sana gari.
“Wamemwambia mambo mengi, hata kuinainama kila mara pia wamekataza. Kimsingi mwenzangu anahitaji uangalizi wa karibu sana. Hata hivyo anaweza kuendelea na filamu ila kwa kuzingatia na scene (onesho) yenyewe, ila kwa sasa anapumzika kwanza ili afya yake itengemae.”

KLINIKI KILA WIKI
Akiendelea kuzungumzia afya ya mumewe, Wastara alisema huwa wanalazimika kwenda Kliniki ya kila wiki katika hospitali moja jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuangaliwa maendeleo yake.
Aidha, alisema kila wiki tatu huwa wanatuma vipimo nchini India katika Hospitali ya Apollo aliyokuwa akitibiwa kwa lengo la kuchunguza maendeleo yake.

KUHUSU UGONJWA WA NGOZI
Wastara alisema, tatizo la ngozi alilonalo mumewe bado hajaanza kutumia dozi yake kwa sababu hawajapata fedha ya kutuma India ili waweze kutumiwa dawa zenyewe.
“Tupo kwenye mchakato wa kutafuta hizo fedha, lakini hali bado ni ngumu na anatakiwa kuanza dozi mapema kama madaktari walivyoshauri,” alisema na kuongeza:
“Mwezi Desemba (mwaka huu) anatakiwa kurudi tena ili aangaliwe tena maendeleo yake kwa ujumla. Yote hiyo ni gharama kubwa sana, lakini tunaamini Mungu atatusimamia.”

GHARAMA ZAMTOA CHOZI WASTARA
Alisema kwa namna mahitaji yalivyo mengi na yanayohitaji fedha, wapo kwenye wakati mgumu kuweza kuyakabili.
“Kiukweli bado tunahitaji msaada wa Watanzania wenzetu. Tunashukuru kwa wale waliojaliwa kutusaidia awali hadi kufanikisha safari yetu ya matibabu India lakini watakaoguswa wanaweza kuendelea kutusaidia.
“Mpaka sasa Sajuki hajaanza dozi ya ugonjwa wa ngozi na zipo nyingine anazotakiwa kuzitumia, lakini hazipatikani hapa...ni mpaka India.”

VIDUME VYAMTOKEA WASTARA
 Akizungumzia suala la usumbufu wa kimapenzi, Wastara alisema ni jambo la kawaida na ni kweli kuna baadhi ya wanaume wanatumia udhaifu wa ugonjwa wa mumewe kumshawishi kimapenzi.
“Kutongozwa ni jambo la kawaida kwa mwanamke, lakini mimi kama Wastara msimamo wangu ni kumheshimu mume wangu. Siwezi kushawishika kwa namna yoyote, kwanza hata hamu yenyewe sina.
“Ninachokiangalia kwa sasa ni afya ya mume wangu. Najua nina wajibu mkubwa wa kuhakikisha namhudumia mume wangu kwa mapenzi yote. Akili yangu haipo kwenye mapenzi kabisa, hali aliyonayo mume wangu inaniumiza sana.
“Kamwe sitamsaliti Sajuki wangu. Wema wake kwangu wakati nikiwa kwenye matatizo siwezi kuulipia kwa kumdhalilisha kwa kutoka na mwanaume mwingine eti kwa sababu anaumwa. Anayewaza kufanya hivyo, akajaribu kwingine, siyo kwangu.”

KALAMU YA MHARIRI
Kwa matatizo aliyonayo Sajuki ni wazi yeye na familia yake bado wanahitaji msaada wa hali na mali ili kuweza kukidhi mahitaji ya matibabu yanayomkabili kwa sasa.
Kama Mtanzania mwenzake, guswa na moyo wa utoaji na Mungu wa Mbinguni atakuongezea katika mifuko yako.
Ikiwa umeguswa, tafadhali tuma mchango wako kwenye akaunti namba 050000003047 yenye jina la Wastara Juma Issa iliyopo katika Benki ya Biashara ya Akiba (ACB) au tumia Tigopesa kwenda namba 0713 666113 yenye jina Wastara Juma.

NDOA YA MWIGIZAJI WA FILAMU ZA KIBONGO DOTNATA YAVUNJIKA


BAADA ya staa wa kitambo katika filamu, Husna Poshi ‘Dotnata’ (pichani) kurudi  katika dini yake ya Kikristo huku akiwa na ndoa ya Kiislamu na mumewe Mohammed Poshi, Sheikh Mohammed Ramadhan wa Msikiti wa Kichangani, Magomeni jijini Dar amesema ndoa ya wawili hao imevunjika.
Akizungumza na Tollywood Newz, jijini Dar es salaam, Sheikh Mohammed alisema kwa sheria ya Kiislam, wawili hao hawana ndoa bali watakuwa wanafanya zinaa.
“Dotnata atakuwa anamtania Mungu kwa kufanya mchezo wa kuzihama dini, lakini namtaka aache kumpikia futari Poshi na hata kama watakuwa wakifanya tendo la ndoa basi wajue  wanachokifanya ni uzinifu tu,” alisema Sheik Mohammed.
Hivi karibuni, Dotnata kupitia  gazeti la Ijumaa alisema kuwa ameamua kurudi katika ukristo na hana tatizo na mumewe kwani wanaendelea kama kawaida.

Sunday, July 22, 2012

FILAMU MPYA YA "DUNIA HAINA HURUMA" INAKUJIA SASA

Mwandishi: Rulea Sanga

Umefika wakati Mungu amezungumza na hawa watumishi wa Mungu kwa kuwapa maono ya kutengeneza filamu ya "Dunia Haina Huruma". Ujumbe huu unatoka katika nyimbo mpya ya mwimbaji maarufu Tanzania, Bahati Bukuku inayoitwa "Dunia haina Huruma" Nyimbo hii imekuwa gumzo jijini Dar es Salaam kutokana na ujumbe wake unaogusa maisha ya watu na kukuweka karibu sana na Mungu unapousikia. Kama hujawahi kuusikia, nakuomba ujitahidi kusikiliza Praise Power Radio na Wapo Radio utabarikiwa.

Mhusikaka mkuu wa filamu hii, Bahati Bukuku

Kutoka na wimbo huu, watumishi wa Mungu wameamua kukaa chini na kuuzambaza ujumbe huu kwa njia ya filamu. Kwahiyo utafaidika kuusikia kwa njia ya uimbaji na pia kwa njia ya maigizo.

Katika filamu hii kutakuwa na watumishi wa Mungu kama James Temu a.k.a Uncle Jimmy (ambaye ni mwigizaji wa filamu Tanzania na ni mtangazaji wa Praise Power Radio Tanzania, mbali na hapo ni blogger) , Rulea Sanga (ambaye ni blogger na ni graphic designer, na mwezi April 2012 alibahatika kuitwa na Nabii TB Joshua kutokana na kazii yake nzuri ya blogu), David Robert (huyu ni muimbaji wa nyimbo za injili Tanzania na ni mjasiliamali mkubwa sana Tanzania), Bahati Bukuku (Huyu ndiye mhusika mkuu wa filamu hii, ni mwimbaji wa nyombo za injili Tanzania na amekuwa baraka kwa wale waliosikia nyimbo zake), Riyama Ally (huyu ni mwigizaji wa filamu Tanzania, amefanya kazi nyingi katika uigizaji)

Wimbo wa Bahati Bukuku wa Dunia haina huruma unagusa sana mioyo ya watu, hasa wale walioko katika ndoa na wale wanaotaka kuingia katika ufalme wa ndoa. Kutokana na wimbo huo, mtumishi wa Mungu Bahati Bukuku akaamua kuja na wazo la kutengeneza filamu ambayo itaonyesha kila kitu alichokiimba katika wimbo huo.

Mshiriki mwingine wa filamu ya "Dunia haina Huruma", Blogger wa RUMA AFRIKA, Rulea Sanga. Hapa akiwa katika gari la Wise Men wa Nabii TB Joshua katika Synagogue ya THE SCOAN. Kumbuka mwezi Aprili 2012 aliitwa na Nabii TB Joshua kutokana na kazi yake nzuri ya blogu yake ya www.rumaafrica.blogspot.com

Kwa sasa kila kitu kuhusina na filamu hii kimeandaliwa, ila kilichobaki ni kumtafuta dada mrembo na mwenye kuvutia, kwani kuna sehemu inahitajika kwaajili ya dada ambaye ni mrembo sana. Kama wewe unajiona ni mrembo na uunajiamini na unaweza kuigiza tunaomba uwasiliane kwa namba hii +255 713-763939.


Kumbukeni haya yote yanafanyika kwaajili ya kumtangaza Kristo na kuonyesha kuwa hata sisi tuliokoka tunaweza kufanya vitu vikali na vizuri. Umefika wakati wa kupenda vilivyo vya Mungu na ku-support kazi ya Mungu. Support yako itatuwezesha kufanya vitu vikali. Mungu anatumia watu kufanikisha kile anachotaka kifanyike, na leo wewe utakuwa ni mmoja wa wale Mungu anapenda ushiriki katika ku-support kazi hii isonge mbele. Kama unamchango wako wowote tutashukuru sana kusikia na kupokea kwako, mchango unaweza ukawa na mawazo, fedha au vitu. Kama wewe ni mmiliki wa vyombo vya shooting unaweza ukajitokeza tukafanya kazi ya Mungu.

Kwa mujibu wa Bahati Bukuku, amesema filamu hii itakuwa ya utofauti na filamu za watu wengine kwani watu watakao shiriki filamu hii watapimwa uwezo wao wakufanya kazi napia watasafiri baadhi ya mikoa kukamilisha kusudio la filamu hii.
Wadau wa blogu hii endeleni kuitembelea, ili mfahamu kitu kinachoendelea.

Riyama Ally ni mtumishi wa Mungu na anacheza filamu za Kitanzania (Bongo Movie). Naye atashiriki katika filamu hii.

David Robert, ni mwimbaji wa nyimbo za injili Tanzania na mjasiliamali. Atashiriki
Uncle Jimmy , ni mwigizaji katika Bongo Movie na amecheza na waigizaji wakubwa Tanzania akiwaomo Ray, JB,O na wengine wengi. Katika filamu hii utaona kazi yake ya uigizaji katika muonekano mwingine.


NIKUPE KIONJO CHA TAMTHILIA

Bahati Bukuku alipigiwa simu na mwanamke mmoja ambaye alijitambuliha kuwa yeye ni mke mwenzake, alimpa taarifa mbaya akimwambia "Nenda kachukue mzoga wako Muhimbili" . Bahati Bukuku akiwa katika kutafuta marafiki zake kuulizia taarifa hizi ili kujua zaidi, aliamua kufika mochwari Muhimbili, na alipofika Muhimbili alikutana na taarifa mbaya za kuumiza moyo wake kutoka kwa wale waliokuwa hapo Muhimbili.
Bahati Bukuku aliingia chumba cha maututi na kuona mpenzi wake amepoteza fahamu na hawezi kumtazama. Nilijisemesha kuwa "Dunia haina huruma, haina fadhili, nani mwenye huruma anifariji, moyo unavuja damu kwa matatizo ninayopata."
Bahati Bukuku akamua kuwapigia ndugu wa mume wake Mbeya ili awaeleze yaliyomsibu, lakini cha kushangaza ni kwamba wote walimsusia. Akajaribu kuchukua kitabu cha Bank ili kuangalia kama kuna pesa kidogo zimsaidie, lakina cha kusikitisha anaona ATM haizomi nikimaanisha hakuna pesa. Hakuchoka akaenda kwa daktari na kutaka kumuuzia gari aina ya Vogi, lakini daktari anakataa na kusema haya magari yanakula mafuta sana kwahiyo sitoweza kuwa nalo. Akiangalia marafiki zake wanazidi kularua moyo wake kwa maneno makali.
Bahati Bukuku kila akimwaangalia mume wake anazidi kuchanganyikiwa na hawezi kuongea naye. Mashemeji zake hawataki kusaidia na kila akiomba msaada kutoka kwao, nao wanamwambia "Shemeji sisi tunaenda kuangalia mpira Ulaya" akiwaambia mawifi zake nao wanamwambia, "Wifi hatuwezi kukusaidia, tunaenda kucheza segere".
Bahati Bukuku akaamua kwenda tena kwa daktari kuomba asaidiwe. Na chanzo cha matatizo kikaanza hapo. Bahati akibdi azae na huyu daktari ili apate msaada, maana amehangaika sana bila ya kupata msaada, na mgonjwa hali yake ni mbaya sana.

Mzigo ukazidi kwa Bahati Bukuku, hali ikazidi kuwa mbaya sana, maana amefanya kosa la kufanya tendo la ndoa na daktari na kuzaa mtoto, na bado ndugu hawampendi.
Baada ya kupata nafuu kwa mgonjwa na kurusiwa nyumbani na kuendelea na maisha yake ya kwaida, Bahati Bukuku akamwambia kuwa nimezaa na daktari. Na hii nililifanya kutokana na kushindwa kupata msaada kutoka kwa ndugu na marafiki, wote walinikimbia, kwahiyo nikaamua kufanya hivyo kwa daktari ili nipate pesa ya kukusaidia upate matibabu.

Mume na Bahati Bukuku aliposikia habari hizo kuwa mke wake ana mtoto na daktari akachukua mapnga na kutaka kumuua.

Mume na Bahati aliondoka na baadae Bahati Bukuku akaitwa kijijini kwa mume wake. Alipofika kijijini akawasalimia, nao hawakuta kumjibu wala kumsikia. Kikao kikakaa kutaka kumhukumu, na wakamwambia Bahati Bukuku, "Kama unataka kuishi katika familia hii, mtoto auawe". Akamtazama mume wake na yeye akamtazama kwa hasira. Bahati aakjiuliza, amkimbile nani kwani ndugu, marafiki na mume wake hawamtaki.
Ndugu wakmuweka mtoto kati ili wampige mapanga, akatokea baba mmoja na kuwauliza, ambaye hana dhambi na awe wa kwanza kupiga panga huyu mtoto. Mume na Bahati Bukuku baada ya kusikia hilo aliomba msamaha kwa mke wake na kusema kuanzia leo hii ya dunia yameisha nataka kutengeneza na Mungu.

Bahati amegundua ya kuwa Mungu anaweza kujibu maombi na kusamehe. Hii ni stori fupi ya tamdhilia ambayo itakujia kwako, kuna mengi ambayo utayaona katika filamu hiyo, Utaona mazingira yatakyotumika, wahusika wanatavyokuwa serious kukuletea huu ujumbe.

Lakini nataka kukuuliza wewe mdau wangu, unafikiri Rulea Sanga, David Robert, Uncle Jimmy, Bahati Bukuku n, Riyama Ally anaweza kufaa katika kitengo kipi?

Kwa haraka haraka kuna wahusika wafuatao:

1. Mke wa yule mume mgonjwa
2. Mume ambaye ni mgonjwa
3. Dada aliyempigia simu mke wa yule mume
4. Marafiki /mashoga wa mke wa mume
5.Daktari
6. Ndugu wa mume
7. Watu waliokataa kumsaidia Bukuku akiwa na shida.
8. Ndugu aliyepigiwa simu na Bahati Bukuku
9. Wacheza segere
9. Ndugu waliomua kwenda Ulaya kuangalia mpira
10. Mtoto wa daktari ambaye aliambiwa akatwe mapanga
11. Mtu aliyewambia wasimkate mapanga
TUNAOMBA MAONI YAKO.

Friday, July 20, 2012

JENNIFER KYAKA (ODAMA) AMEFIWA LEO NA MAMA YAKE MDOGO

Muigizaji wa filamu Tanzania Jennifer Kyaka (Odama) leo asubuhi amefiwa na mama yake mdogo katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam. Marehemu alikuwa amelazwa mahali pale kwa muda mrefu sana, lakini leo Mungu amempenda na  amemuchukua.Sasa hivi zinafanyika jitihada za kuondoa mwili wa marehemu n kuelekea nyumbani kwake. Tutazidi kuwajuza ni wapi msiba utakuwepo.


Unaweza kuwasiliana na Jennifer Kyaka kwa kutembelea blogu yake ya www.odama1.blogspot.com

Sunday, July 15, 2012

UZINDUZI WA ALBAM YAAHAKUNA JIPYA YA EMMANUEL MGAYA "MASAJNA" WAFANA-IRINNGA

Mungu alimtumia Emmanuel Mgaya (Masanja Mkandamizaji au Mchungaji Mtarajiwa) kuwakusanya watu katika Uwanja wa Samora mjini Iringa kushuhudia matendo makuu ya Mungu, ambapo msanii huyu alikuwa akizindua albamu yake ya "Hakuna Jipya" Masanja Mkandamizaji ni mkazi wa jijini Dar es Salaam ni mzawaliwa wa mkoa wa Iringa. Aliamua kufanya tamasha lake katika mkoa aliozaliwa.

Msanja Mkandamizaji aliwakusanya watu kutoka mikoa mbalimbali waliofika  kushuhudia uzinduzi huo. Wasanii wa filamu za kibongo kutoka Dar es Salaam walifika mahali pale kama. Odama, Ray, steve Nyerere, Davina, Chopa Mchopanga, Jacquline Wolper na wengine wengi walifika mahali pale.

Mbali na uimbaji masanja Mkandamizaji ni mchekeshaji katika kituo cha televisheni cha TBC1 "Orijino ze Commedy", kutokana na karama hiyo ya uchekeshaji amepata kibali cha kukubalika katika jamii.

Masanja kwa sasa anajiita "Mchungaji Mtarajiwa" anategemea kuwa mchungaji lakini anasema hajui itakuwa saa ngapi, siku gani na wapi ataanza huduma hiyo, ila anakuomba uzidi kumuombea.

Masanja akisindikizwa na waimbaji mbalimbali kutoka Iringa na mikoa mingine katika uwanja wa samora mjini Iringa

Masanja Makadamizaji akikagua gwaride lake

Masanja Mkandamizaji na gwaride lake wakiingia jukwaani

Waimbaji wakiwa pamoja na Masanja Mkandamizaji aliyeshika ubao kama alama ya bunduki
Diwani wa kata ya kitanzini Manispaa ya Iringa Jesca hakuwa nyuma kutoa support kwa kununua DVD ya album ya HAKUNA JIPYA


JB toka bongo movie akitoa support kwa kununua DVD na Audio Cd

Hapa Mgeni Rasmi akiongea baada ya kuzindua waliokaa ni baadhi ya wabunge wa viti maalum na mkuu wa mkoa wa Iringa.


Tayari hapa Mgeni rasmi Mulugo amsehazindua


Naibu Waziri wa Elimu Milubo akizindua DVD na VCD


Baadhi ya viongozi wa Elimu wakiwa na mgeni Rasmi

Kundi la Bongo Movie kutoka Dar es Salaam waliofika ku-support kazi ya Emmanuel Mgaya

JB wa Bongo Movie akiwa ameshika kibaza sauti pamoja na waigizaji wenzake

Jacquline Waolper akiwa na furaha kuona tamasha linaenda vizuri


Vicent Kigosi (Ray) akisalimia wakazi wa Iringa


Steve Nyerere akitambulisha wakazi wa Iringa kikundi cha Bongo Movie

Masanja Mkandamizaji akisoma risala
Mke wa blogger Fracis Godwin wa Iringa akiwa na mwanae Falavian

Martha Baraka akimzindikiza mwimbaji mwezake MasanjaMwimbaji wa nyimbo za injili Martha Mwaipaja akimtumikia BWANA


Watu waliohudhuria tamasha hilo uwanja wa Samora mjini Iringa wakati wa tamasha la Emmanuel Mgaya


Hotel ya Blue View na Fan Lodge ndio wadhamini wa tamasha hili