SARAH K LISEME SONG

Thursday, January 12, 2012

MWANASOKA WA ZAMANI,, KITWANA MANARA AFIWA NA MAMA YAKE
Mwanasoka nyota wa zamani wa timu ya Taifa, Kitwana Manara, amefiwa na mama yake mzazi, Bi. Mishi Mikessy (pichani) jana usiku jijini Dar es Salaam.

Kitwana amesema mjini Dar es Salaam leo kuwa, mama yake huyo, anayekadiriwa kuwa na umri wa zaidi ya miaka 95, alifariki dunia baada ya kuugua kwa wiki kadhaa.

Kwa mujibu wa Kitwana, mazishi ya Bi Mishi yanatarajiwa kufanyika kesho katika makaburi ya Waanglikana yaliyopo Buguruni-Malapa, jijini Dar es Salaam.

Marehemu Bi. Mishi ameacha watoto watano na wajukuu kadhaa.
Kitwana ni kaka wa wanasoka wengine nyota wa zamani nchini, Sunday Manara na Kassim Manara.

Mkongwe huyo wa soka nchini, aliyezichezea klabu za Yanga, Pan African na Taifa Stars, anaomba taarifa hizi ziwafikie ndugu na jamaa popote walipo duniani.

Mungu aiweke Roho ya Marehemu Mahala pema Peponi.

-Amin

No comments:

Post a Comment