FAMILY DAY BONANZA YAWAPAGAWISHA TIP TOP CONNECTION, TOT NA MSONDONGOMA DAR LIVE MBAGALA-
Mnenguaji wa TOT, Halima Said ‘Queen Emmy’, akionyesha ukali wake wa nyonga.
Wanamuziki wa Msondo Ngoma, Hassan Moshi ‘TX Junior’ (kushoto), Maalim Gurumo na Shabani Dede , wakishabulia jukwaa.
Kiongozi wa kundi la TIP TOP Connection Ahmed Ally ‘Madee’ akitumbuiza.
-----------------------
KUNDI la Tip Top Connection la Manzese jijini Dar es Salaam, Bendi ya Msondo Ngoma na kundi la Tanzania One Theater ‘TOT’ lililo chini ya malkia wa mipasho Bongo, Khadija Kopa, jana waling’ara vilivyo katika Ukumbi wa Dar Live Mbagala jijini Dar es Salaam, katika shoo zao za kwanza kufanyikia ndani ya ukumbi huo wa mashabiki kibao.
Shoo hiyo iliyokuwa imefurika umati wa wasaka burudani tangu mishale ya saa tano asubuhi ilijumuisha ngoma za asili na wasnii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Mbagala walioonyesha umahiri wao bila ajzi.
Msondo Ngoma ndiyo ilianza na ikafuatiwa na TOT ambapo pazia lilifungwa na TIP TOP Connection.
No comments:
Post a Comment