WATANZANIA MNAOMBWA KUJITOKEZA KATIKA MKESHA MKUBWA WA KULIOMBE TAIFA Desemba 31, 2011
Na Emmanuel Kimweri
Umoja wa Makanisa ya Kikristo Tanzania (Tanzania ChristianFellowship of Churches) umeandaa mkesha mkubwa kwa ajili ya dua maalum kwa taifa kwa lengo la kumshukuru Mungu kwa kulivusha Taifa katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru,sambamba na kupongeza msimamo wa serikali wa kupinga maswala ya ushoga.
Mkesha huo Mkubwa wa kuliombea Taifa mgeni rasmi katika mkesha huo anatarajia kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Mwenyekiti wa Kamatai ya Mkesha wa kuliombea Taiafa ambaye pia ni Askofu wa Tanzania Fellowship of Churches, Godfrey Emmanuel Malassy akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es sa Salaam
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Mkesha mkuu kutoka Tanzania Christian Fellowship of Churches Askofu Godfrey Emmmanuel Malasi, alisema tunawaomba watanzania kujitokeza kwa wingi katika kuliombea Taifa letu la Tanzania kwa kufikia mikaka 50 ya Uhuru na kuukaribisha miaka mingine 50 bila machauko kwa Tanzania yetu ya amani..
“Kila mmoja anapaswa kushiriki na kushirikishwa kikamilifu katika uchumi wa taifa letu ambalo sasa limemaliza miaka 50 ya uhuru, kila mtu anapaswa kutambua nafasi yake, tusikae kwa kubweteka, tusikae kwa kulalamika kila mtu ajue ni wakati wa kumiki na kurithishwa rasilimali zilizopo katika taifa hili” alisema
Alisema mwaka huu dua maalum kwa taifa litafanyika katika mikoa 14 ya Tanzania ikiwemo Dar es salaam, Arusha, Mwanza,Kilimanjaro, Singida Iringa, Mbeya ,Iringa, Kagera, Dodoma, Ruvuma, Tabora,Tanga na visiwa vya Zanzbar na Pemba.
Amefafanua kuwa katika mkesha huo viongozi mbalimbali wa taifa ,na wavyama vya siasa na balozi mbalimbali zipatazo 37 zilizopo nchini zimearikwa kushiriki mkesha huo na kuongeza kuwa tayari baadhi ya balozi zimethibitisha kushiriki katika mkesha huo.
“ kwa kuwa miaka ya 50 ya Taifa letu imetimia mkesha wa mwaka huu utaambatana na tukio maalum la watoto 50 kusimama uwanjani na kutamka maneno ya kupokea miaka 50 ijayo ikiwa ni ishara ya kupokea kizazi huru cha watanzania.
No comments:
Post a Comment