SARAH K LISEME SONG

Thursday, December 29, 2011

MTANGAZAJI WA TBC TAIFA, BI. HALIMA MCHUKA AFARIKI DUNIA

MTANGAZAJI Bi. Halima Mchuka wa muda mrefu wa iliyokuwa Redio Tanzania Dar esSalaam RTD na baadae Shirika la Utangazaji Tanzania (SHIUTA) amefariki Dunia.

Taarifa zilizopatikana hivi punde zinadai kuwa Mtangazaji huyo ambaye alikuwa na kipaji kikubwa cha utangazaji  amefariki Usiku huu wa leo tarehe 29-12-2011 saa 9.00alfajiri kutokana nakupatwa na stroke ya gafla .

“Alikuwa na tatizo hilo jana mchana mara baada ya kutangaza kipindi cha salaam cha TBC-Taifa na akazidiwa ndipo alipopelekwa Hospitali na sasa ndiyo amefariki dunia.”alibainisha mmoja wa watangazaji wa TBC ambaye alikuwa jirani na mtangazji huyu.

Halima Mchuka alijiunga na Radio Tanzania Dar es Salaam mwaka 1994 ambapo alifanya kazi katika idara ya Habari na idara ya mipango.

Wadau wengi wa RTD na baadae TBC-Taifa wanamkumbuka sana mama huyu wa watoto wawili kwakuwa mwanamke wa awali kuangaza mpira katika ukanda wetu huu wa Afrika Mashariki na kati.

“Unapotaja mpira wa miguu wakai huu huwezi kusahau kipindi cha michezo cha RTD cha saa mbili kasorobo na huyu dada Halima Mchuka.”alibainisha Idd Pazi mmojawapo wachezaji nguli wa Tanzania wa wakati huo.

Kwa hakika si wasikilizaji wa RTD na wanamichezo tu bali ata watu wa Karibu ambao waliwahi kufanya nae kazi tunamtazama kuwa ni mtu mpole mwenye huruma na kusaidia wenzake pale penye tatizo ambalo yeye anaweza kulitatua.

Mungu ailaze Roho ya BI Halima Mchuka pahala pema peponi Amina

No comments:

Post a Comment