SARAH K LISEME SONG

Wednesday, July 11, 2012

FILAMU YA KUMCHANGIA SAJUKI NA MKE WAKE IITWAE SYLA KUZINDULIWA



Tarehe 13 Mwezi wa Saba, 2012 katika jiji la Arusha, filamu ya SAYLA itazinduliwa rasmi. Filamu hiyo iliyoshirikisha wasanii na watu maarufu takribani 27 ilirekodiwa maalum kwa ajili ya kuonyesha kuwa kwa kutumia sanaa, sisi watanzania tunaweza kusaidiana wakati wa matatizo.




Filamu hii maalum kwa ajili ya kuwasaidia Sajuki na Wastara waliokuwa katika wakati mgumu wa kutafuta pesa za matibabu, itazinduliwa kwenye ukumbi wa Naura Springs na kuhudhuriwa na watu wengi maarufu nchini akiwemo Mh Shyrose Bhanji na wabunge wengine wa Bunge la Afrika Mashariki, Wema Sepetu akiongoza kundi la wasanii wa Bongo Movie pamoja na wengine kama Snura, Shilole ambao watatumbuiza kwa kushirikiana na Ndege mnana Linah, kwa mara ya kwanza jijini Arusha toka adondoke.

SAYLA ni filamu ya kihistoria iliyoshirikisha idadi ya kubwa ya mastaa kuliko yeyote ile, itazinduliwa pamoja na video na behind the scene za nyimbo ya Mboni yangu!

Baadhi ya watu walioshiriki kwenye hiyo project ni kama ifuatavyo: Mh Zitto Kabwe, Mh January Makamba, Mh Halima Mdee, Mh Esther Bulaya, Mh Vicky Kamata, Mh Shyrose Bhanji, Mzee Chillo, Mzee Hashim Kambi, Muhogo Mchungu, Bi Kidude, Sharo Milionea, Mboto, Kitale, Wema Sepetu, Davina, Ephrahim Kibonde, Adam Mchomvu, Arnold Kayanda, George Goyayi, Mairmatha wa Jesse, Rose Chitala, Ruben Ndege, Irene Paul, Dully Sykes, Chege, Madee, Recho, Ommy Dimples, William Mtitu, Mwana FA na wengine wengi.

Filamu hiyo imetayarishwa na timu kubwa ya waandaji wakiwemo William Mtitu, Simon Mwakifamba, Zamaradi Mketema pamoja na Shamim (8020 blogspot.com).

Tusikose kwenye uzinduzi huu wa hadhi ya kimataifa ambapo kwa mara ya kwanza jijini Arusha, wageni watapita kwenye REd carpet maalum.

Kiingilio ni Shs 20,000/= na Shs 10,000/- viti vya kawaida. Na filamu inategemewa kuanza saa 3 kamili usiku katika ukumbi wa Naura Springs.

Monday, July 2, 2012

BWM X6 YA MWIGIZAJI WA BONGO MOVIE -JACKQULINE WOLPER LAKAMATWA




LILE gari la kifahari aina ya BMW X6 lenye namba za usajili T 574 BXF linalomilikiwa na staa wa sinema za Bongo, Jacqueline Wolper Masawe limedakwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Kwa mujibu wa ofisa mmoja wa TRA ambaye hakutaka jina lake lichorwe gazetini, gari hilo la kisasa lilikamatwa Juni 28, 2012 kupitia Kampuni ya Mnada ya Majembe kutokana na sababu kadha wa kadha.

SABABU ZAANIKWA
Akiendelea kufunguka, afisa huyo alisema kuwa sababu ya kwanza ni kuhisiwa kuwa gari hilo liliingizwa nchini kinyemela kutokana na vielelezo vyake vya kwenye kadi kupitia kwenye vyombo vya habari, ndipo taa nyekundu ikawaka ndani ya vichwa vya maafisa wa TRA na kuanza kulifuatilia.
Alidai kuwa mbali ya kuingia nchini kinyemela, lakini BMW hilo halijalipiwa ushuru zaidi ya miaka mitano iliyopita kwa mujibu wa vielelezo vyake.

MPANGO WA KULIKAMATA ULIVYOSUKWA
Kwa mujibu wa ofisa huyo, ili kufanikisha zoezi la kulikamata gari hilo, vijana kutoka kampuni ya Majembe waliingia mzigoni kulisaka ambapo kuna mtu alipiga kambi jirani na makazi ya Wolper, Mbezi Beach jijini Dar.
Ilisemekana kuwa vijana hao walikuwa na kazi moja tu, kuhakikisha anapotoka Jack wanamfuatilia hatua kwa hatua hadi mahali atakapokwenda kupiga kambi na kulitia mikononi.
“Haikuwa kazi rahisi maana muda mrefu alikuwa haonekani nalo, ndipo mpango huo ulipokuja kukamilishwa kwa njia ya kumfuatilia anapotoka kwake hadi mahali lilipokamatwa maeneo ya katikati ya Jiji la Dar,” alisema.

Akaendelea kudai: “Unajua hawa mastaa wetu kuna vitu wanavifanya bila kujua madhara yake, kitendo cha Wolper kuonesha kadi ya gari kwa waandishi wa habari huku anafahamu ina mapungufu kibao ndiyo sababu kuu ya gari hilo kuanza kufuatiliwa.”

MH! ETI USHURU MILIONI 70?
Taarifa nyingine ya kushtua ni kwamba ilidaiwa kuwa kuwa TRA peke yake inadai Sh. milioni 70 za ushuru.
“Si fedha ndogo zinazodaiwa na TRA, kwa hesabu ya harakaharaka ni zaidi ya Sh. milioni 70 ambazo zinatakiwa kulipwa.”
Baada ya The Biggest IQ Paper, Ijumaa Wikienda kujiridhisha kuwa gari hilo limedakwa, lilimuendea hewani Wolper lakini hakuweza kupokea simu hadi gazeti linakwenda mitamboni.

Chanzo-http://networkedblogs.com at 7/02/2012 03:11:00 AM

Sunday, July 1, 2012

FLORAH MVUNGI AKIMCHANA IRENE UWOYA AMWITA SCRAPER KISA H-BABA..

 
ALICHO KIANDIKA FACEBOOK KWA WALL YAKE ni HIKI..... Florah Mvungi ujumbe huu umeletwa kwako na florah mvungi and salma jabu nishabebe.kuishi na bwana kunahitaji ufundi,kama hujafundwa kwenu unakurupuka utajibeba.,mwanamke huna heshima kutwa kulala na wanaume
wa kila aina nani atakutaka?wanaokutaka hawana nia na wewe wanakuonja tu.ukome kufuatilia mapenzi yetu wenyewe tumeridhika na maisha yetu ,umeona haitoshi yote uliyoyafanya yamegonga mwamba umeona useme oo bwana hajui mapenzi inahusu nini ?wewe ndo hujui bibi ndo mana hutulii na wanaume kila mtu akufunue we mwanamke gani usiyejali utu wako?ndoa imekushinda kkisa umalaya ,,yetu yaache hayakuhusu ulimuona hafai ukaleta vitimbi bwana kakuacha hakutaki hashuo za nini?wewe IYANA UWAYA ukome,.roho inakuuma kuona napendwa raha ulizoziona za nini napewa mie kwa raha zangu linakuuma ,.fanya yako o ushakuwa scaper,.kama mpira wa kona unaona unashuka unatafuta bifu na mie ili upande ntashindwa mie DECENT GIRLbwana nathamini utu wangu wala sidanganyiki kwa vijisenti vya wapita njia. chanzo -Teen tz

Saturday, June 30, 2012

UZINDUZI WA SOBBING SOUND NA WATOTO YATIMA

Source: Ray The Greatest

Hatimaye mzigo wa Sobbing Sound umeingia mtaani kwa aina yake baada ya kaumua kwenda kuizindua na watoto yatima wa kituo cha Maunga kilichopo maneno ya Kinondoni studio, Kwanini nimeamua kufanya hivi wadau ni kwa sababu nimeguswa na jinsi wanayoishi watoto yatima katika mazingira magumu ili ni jukumu la Watanzania wote kuanza kuguswa katika hili maana hapa duniani sisi ni wapangaji tu makazi yetu ni kwa Mungu Baba sasa unapopata kidogo jaribu kuwafikiria na wale waliokuwa na maisha magumu, yani tugawane umasikini. wadau sikuwa na kikubwa sana ila nimejitolea pale nilipoweza kubarikiwa na Mungu Baba unaambiwa kuwa kama utoweza kushukuru kwa kidogo basi hata ukipata kikubwa pia utakuwa mgumu kumshukuru yule aliyekuwezesha kukupa kipato hicho...



Hivi ni baadhi ya vitu nilivyowapelekea watoto wa kituo hicho wadau kutoa si utajiri bali ni moyo na nimeamua kila sinema yangu inapotoka basi lazima nirudishe shukrani zangu kwa Watanzania wa hali ya chini nitaanzia Dar es salaa na baadaye mikoani wadau ..



Watoto wa kituo hicho wakiwa wametulia kufuatilia kinachoendelea..



Waandishi wa habari kutoka vituo tofauti walikuwepo kuchukua habari kama kawaida ya wanahabari panapokuwa kuna tukio.



Pritesh toka Steps kampuni ya usambazaji hapa nchini alikuwepo kunipa tafu katika jambo ili la kuwasaidia watoto yatima..







The Greatest(Ray) nikiwa nimewasili katika kituo cha watoto yatima cha Maunga nikimsikiliza mama mlezi wa kituo hicho.

Mama mlezi wa kituo hicho akiongea machache pamoja na kunishukuru.


Nami nilipata fursa ya kuongea ya kwangu.



Zoezi la makabhiano yalianza kama ifuatavyo, hapa nikimkabidhi Mama mlezi kiroba cha unga..



Mambo yakiendelea...



Nikiendelea na taratibu za kutoa msaada.



Niliweza kutembelea maeneo wanapolala ndugu zangu na kama mnavyoona wadau tunahitaji kujitoa kuwasaidia ndugu zetu..




Na hichi ndio choo chao embu angalieni jamani hii n hatari sana kama utakuwa na chochote ama umeguswa kusaidia basi tunaweza kuwasiliana.

Baada ya matukio yote nilipewa nafasi nyingine ya kusaini kitabu cha wageni.


Niliweza kupata picha ya pamoja na watoto hao.


Hapa nikiongea na vyombo vya habari..


Nikipokea shukurani yao.




`Nilifurahi sana kwa kupata nafasi kubwa ya kufika katika kituo cha watoto yatima na hapa wakinisindikiza.

Friday, June 22, 2012

MAINDA SASA ASIMAMA KAMA DIRECTOR


Sasa nimeamua kusimama kama muigizaji na director kwenye movie.Baada ya kimya cha muda mrefu sasa nimerudi na nguvu mpya

Thursday, June 21, 2012

SMALLBABY NARUDI KWA KASI MPYA NA MUONEKANO MPYA

 m                               smallbaby nikiwajibika nikiwa na Nisha na Msungu
 s                               Smalllbaby na Msungu
smallbaby mainda naFrola mvungi
                                             Mainda on Set
                                                  Nikijikumbusha jambo kabla sijaingia on set
 
                                                    Mainda na Shamsha
                                                  Mainda na Jack
Mainda, Smsha, Dullah, Baga

KATIKA KAZI RAZIMA KUWE NAMAADUI

Katika kazi yangu razima iwe na marafiki a maadui hinyo niko tayari  kuwapokea wote wala siogopi adui coz najua baba yangu wa mbinguni yupo upande wangu,hatoniacha adui anidhuru.

Saturday, June 16, 2012

MCHEZASINEMA MAARUFU TOKA MAREKANI KUKIMBIA MBIO ZA MT. KILI MARATHON


Mcheza sinema maarufu duniani kutoka nchini Marekani Deidre Lorenz atakimbia mbio za kila mwaka za Mount Kilimanjaro Marathon zinazoanza kutimua vumbi kuanzia tarehe 24 Juni mwaka huu kutoka Moshi Club mjini Moshi.
Mbio hizi zilizoanzishwa na mama Marie France kutoka katika mji wa Bethesda, Maryland nchini Marekani mwaka 1991 ni mbio zinazojulikana kama 7 continental Races na zimeshawahi kupata tuzo mbalimbali za kimataifa.

Ujio wa mcheza sinema huyu aliyecheza sinema nyingi kama vile Santorini Blue, Perfect Strangers, The Great Fight, na nyingine nyingi unaiweka Tanzania katika macho ya dunia na kuwavutia watalii wengi kutoka taifa hili tajiri duniani. Deidre Lorenz alizaliwa katika jiji la Oregon nchini Marekani lakini akahamia katika jiji la New York City linalijulikana kama "The Big Apple" nchini Marekani akiwa na kampuni yake ya kutengeneza sinema inayoitwa Thira Films LLS.

eidre Lorenz ameshawahi kuteuliwa zaidi ya mara tatu kugombe tuzo za wacheza sinema maarufu duniani zinazojulikana kama Grammy Awards. Mcheza sinema huyu ataambatana na Wamarekani wengine kuja nchini tarehe 21 Juni kukimbia mbio hizi ambazo zimetokea kuutangaza sana mji wa Moshi tangu mwaka 1991. Lorenz alipatikana katika bahati nasibu iliyochezwa wakati wa mbio za New York Marathon mwaka jana.

Naye mwanzilishi wa mbio hizi mama Marie Frances ana historia ya kuanzisha mbio na matamasha mbalimbali duniani. Alikuwa pia mwanzilishi wa mbio za Pyramid Marathon nchini Misri pamoja na Miss Universe Egypt matamasha yaliyojizolea sifa kemkem.Aliombwa kuja kuanzisha mbio za Marathon nchini Tanzania na balozi wa Tanzania wa wakati ule nchini Misri.Mbio za Mt. Kilimahjaro Marathon ni moja kati ya mbio tafauti za marathon zinazifanyika katika mji wa Moshi.

Mount Kilimanjaro Marathon zitaanzia Moshi Club mpaka Rau madukani na kurudi mara tatu ambazo zitakuwa kilimeta 42. Kutakuwa pia na mbio z akilometa 21, kilimeta 10 na kilometa 5 kwa watoto. Wakimbiaji hawahitaji kuwa na ujuzi wa kukimbia watu wote wanaweza kukimbia.

Thursday, June 14, 2012

BANTU FILM AWARDS

Kilio cha muda mrefu cha wasanii wa Tanzania sasa kimefika kikomo baada ya wadau kujitokeza na kuanzisha tuzo ambazo zinaitwa Bantu Film Awards zinategemewa kufanyika mwezi ujao katikati tarehe na siku tutawajuliisha kupitia blog yako ya The Greatest, leo kulifanyika mkutano na waandishi wa habari katika hotel ya Serena kuzungumzia tuzo hizo, embu twende tuone mambo yalivyokuwa.....

Wasanii wa Bongo Movie wakiwa tayari kuanza mkutano na waandishi wa habari.

The Greatest, Richie na Jb wakimfuatilia mratibu wa tuzo za Bantu Film awards bwana Stewart akifafanua jinsi tuzo zitakavyokuwa

Irene Uwoya naye alikuwepo amesema kuwa amepania kuzoa tuzo za mwaka huu..

Tukiwa makini kufatilia kikao na mambo yatakavyokuwa.
Stewart ndiye Mratibu wa Bantu Film Awards
Stewart akiendelea kutoa ufafanuzi jinsi tuzo za Bantu zitakavyokuwa kwa waandishi wa habari
Safi sana kwa kweli wasanii wa Tanzania tumekuwa na faraja kubwa juu ya tuzo hizi za Bantu
Mambo yakiendelea........
Jb mwenyekiti wa Bongo Movie
The Greatest
Irene Uwoya
Single Mtambalike
Ulifika muda wa Jb kuongea yake machache kuhusu tuzo za Bantu, Kubwa alisisitiza kuwa umefika muda sasa ya wasanii kufanya kazi zenye ubora wa Kimataifa maana hiki ndicho kilkuwa kilio chetu cha muda mrefu sana maana hata wanafunzi wanapokuwa wanasoma lazima mwisho wa mwaka ukifika wanafanya mitihani kama kipimo cha mwaka mzima alichosoma na ndio maana leo nasi tumekuwa na kitu kama hiki cha kujipima kuwa ndani ya mwaka mzima umefanya kitu gani.
Hayo yalikuwa ni maneno ya Jb akiwawakilisha wasanii wa Tanzania nzima..
Waandishi wa habari wakifanya kazi zao kama kawaida yao
Mambo yakiendelea kupamba moto
Irene Uwoya naye akiongea yake machache
Single Mtambalike (Richie) naye akiongea mambo ya msingi yanayotakiwa kuzingatiwa katika tuzo hizo
Ulifika muda wa maswali na majibu toka kwa waandishi wa habari
Nikisikiliza swali toka kwa mwaandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi...
Mratibu akilijibu swali ilo kwa ufasaha
Waandishi wa habari wakisiliza jibu kwa ufasaha
Maswali yakiendelea kuulizwa kikubwa waandishi walikuwa wanataka kujua ni vigezo vipi vitakavyotumika kuwachagua watakaokuwa bora kwa mwaka huu