SARAH K LISEME SONG

Monday, April 30, 2012KAJALA AMWAGA CHOZI KORTINI

Happiness Katabazi

MSANII wa Filamu nchini, Kalaja Masanja leo alimwaga machozi na kuuujia juu upande wa Jamhuri katika kesi inayomkabili ya utakajitishaji fedha haramu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, akiushinikiza ulete mashahidi haraka kwani kule gerezani anakoishi siyo sehemu ya starehe.
Kajala alitoa shinikizo hilo jana mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo muda mfupi baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rsuhwa (PCCB), Swai kuikumbukusha mahakama kuwa kesi hiyo ilikuja jana kwaajili ya mashahidi wa upande wa Jamhuri kuanza kutoa ushahidi wao lakini akadai hilo halitaweza kufanyika kwasababu hajaja na mashahidi na kwamba anaiomba kesi hiyo iarishwe.

Baada ya wakili huyo wa PCCB kumaliza kutoa maelezo hayo ndipo Kajala akanyosha kidole na kuomba ruhusa ya mahakama ili aweze kuzungumza jambo na alizungumza kama ifuatavyo:
“Mweshimiwa hakimu hivi huyu wakili wa serikali anafikiri kule gereza la Segerea ninakoishi kwa sasa ni sehemu ya stahere? Gerezani kunatisha wewe wakili wa serikali lete mashahidi kesi isikilizwe”alidai Kajala huku akitokwa na machozi.

Kwa upande wake Hakimu Fimbo aliarisha kesi hiyo Mei 9 mwaka huu,ambapo upande wa jamhuri unatakiwa ulete mashahidi wake ili waanze kutoa ushihidi.

Machi 27 mwaka huu, ilidaiwa na wakili Swai kuwa Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Leonard Swai alidai mbali na Kajala mshtakiwa mwingine ni muwe Faraja Chambo wanakabiliwa na makosa matatu, kosa la kwanza ni la kula njama kinyume na kifungu cha 34 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007 ambapo washtakiwa wote kwa pamoja walitenda kosa hilo la kula njama la kuamisha umiliki wa nyumba iliyopo Kunduchi Salasala eneo ambalo halijapimwa jijini Dar es Salaam. 

Shtaka la pili ni ni kwamba Aprili 14 mwaka 2010 waliamisha isivyo halali umiliki wa nyumba hiyo ambayo walikuwa wakiimiliki kwenda kwa Emilian Rugalia ambaye ndiyo walimuuzia kinyume na kifungu cha 34(2)A(3) cha Sheria ya TAKUKURU ya mwaka 2007. Na shtaka la tatu ni la kutakatisha fedha ambalo walilitenda siku hiyo ya Aprili 14 mwaka 2010 huku wakijiua ni kinyume na sheria hiyo. 

Chambo ambaye naye yupo gerezani kwa zaidi ya mwaka mmoja kwasababu anakabiliwa na kesi nyingine ya utakatishaji fedha haramu iliyofunguliwa mahakamani hapo ambapo kwa mujibu wa sheria kosa hilo halina dhamana.

Source: mamapipiro.blogspot.com

Saturday, April 28, 2012


MCHEZA FILAMU ZA KIBABE ARNOLD SCHWARZNEGGER KUTENGENEZA SANAMU YAKE

Mcheza filamu za kibabe Arnold Schwarznegger ameamua kutengeneza sanamu zinazoonyesha alivyokuwa mtu mwenye misuli enzi zake za uigizaji huo
Katika kufanya hivyo mbabe huyo ambaye aliwahi kuwa Gavana wa Jimbo la California,anataka kuudhirishia ulimwengu kuwa alikuwa shujaa na anastahili heshima
Schwarzegger 64 a meagiza kutengenezwa sanamu tatu za madini ya fedha zenye urefu wa futi nane kila moja.sanamu hizo zinaonyesha alivyokuwa mtu alijengeka vyema kimwili

MWIGIZAJI WA FILAMU NCHINI TANZANIA, JENNIFER KYAKA "ODAMA" AMEFUNGUA BLOG YAKE MPYA INAYOENDA KWA JINA LA www.odama1.blogspot.com
Blogu hii iko katika kiwango cha kimataifa na lengo la kufungua blogu hii ni kutaka kutangaza kazi zake za filamu pamoja na kampuni yake ya J-Film 4 Life ambayo inajishughulisha na utengenezaji wa filamu na kukodesha vifaa vya shooting.
Mbali na hayo, Jennifer amesema atakuwa anaweka habari za wacheza filamu wa Tanzania na nchi nyingine ili wewe upate kujua kinachoaajili katika ulimwengu wa filamu.
Blogu yake imetengenezwa na Blogger Rulea Sanga ambaye unaweza kuwasiliana naye kwa simu +255 715 85 15 23, Email: rumatz2011@yahoo.com, Blog: www.rumaafrica.blogspot.com

SASA NAOMBA UKAANGALIE BLOG YA ODAMA

Friday, April 27, 2012


SHUKRANI ZA PEKEE ZIENDE KWA WOTE WANAOGUSWA NA TATIZO LA SAJUKI
Juzi jumatano nilirusha mahojiano niliyoyafanya na Wastara kuhusu ugonjwa wa msanii Sajuki ambae ni mumewe.Sajuki anasumbuliwa na uvimbe tumboni toka mwaka jana mwezi wa saba.Kupitia leo tena ya clouds fm wengi mlisikia na mkaguswa kuwa sehemu ya wale wanaochangia kumwezesha Sajuki kupata matibabu nchini India mwezi ujao.

Kabla sijaanza kampeni hii nilikutana na Wastara akanieleza hali waliyokuwa nayo.Nikaongea na mkuu wa vipindi clouds fm kwamba tufanye kitu tusiishie tu kutoa taarifa akakubali na ndio maana niliiweka hewani katika leo tena.Kwa mtu yoyote mwenye huruma na imani akimsikia huyu dada lazima alie.Hata juzi wakati nafanya kipindi nikiwa hapa Dodoma nilishindwa kujizuia kulia.Niliweka nadhiri moyoni mwangu na Mungu wangu kuwa kama ni yeye alitaka niwe Dina Marios basi sauti yangu na isikike na lengo la kupata pesa ya matibabu ya huyu kijana ipatikane.Na kweli baada ya kufanya tu kipindi kikaisha kuna mama amejitolea tiketi ya ndege ya kwenda na kurudi ya watu wawili.Watu mbalimbali wamejitokeza kuchangia na pia wengi wamejiunga nami katika kampeni hii akiwemo Shamim Mwasha wa 8020 blog,Joyce Kiria wa wanawake live na wengine wengi.

Pia shukrani za pekee zimwendee mbunge wa viti maalum vijana mheshimiwa Esta Bulaya ambae baada ya kuongea nae ameguswa na tunaenda katika ngazi ya juu zaidi kupata tunachokitaka.Kwa sasa tunajaribu kuipeleka kwa waziri wa vijana utamaduni sanaa na michezo Dr.Emmanuel Nchimbi.Kwa lolote endelea kusikiliza clouds fm the people station.

Bado unaweza kuchangia kwa Mpesa 0762189592 na kupitia Akiba commercial bank acount no 050000003047 Wastara Juma.

Wednesday, April 25, 2012

HONGERA SAJUKI NA WASTARA

 Familia husatawishwa na upendo kati ya baba na mama, na mtoto huwa ni chachu ya furaha katika nyumba
    Hongera sana Sajuki na Wastara, Mungu awape Maisha marefu na muishi kwa upendo na furaha

 Huyu ndiye Mama mtoto(Wastara) akiwa na mwanae na baadhi ya watoto waliohudhuria sherehe hiyo

 Sajuki ambaye ndiye baba wa mtoto akimwangalia mwanawe kwa furaha.

 Irene Uwoya ni mmoja ya wasanii maarufu Tanzania walioweza kufika katika tukio hilo.

 Baadhi ya wasanii wa Bongo Movie wakiwa katika tafrija hiyo.

 Shughuli za kumwangalia mtoto zikiwa zinaendelea

 Recho Haule.

 Kupa mwenye fulana nyekundu akiwa anafuatilia kwa umakini wakati shughuli zikiwa zinaendelea.

 Wasanii mbalimbali.

 Sajuki wa katikati akiwa na wasanii baadhi wa Bongo Movie.

Sajuki akiwa na wana familia wa Bongo Movie.TAMKO RASMI KUHUSU SHUTUMA DHIDI YANGU JUU YA KIFO CHA KANUMBA

Yapata wiki tatu sasa tangu msanii mwenzangu Steven Kanumba aage dunia, na kama ilivyo kwa kila kitu kinapotokea huandamana na kila aina ya maneno na hisia mbali mbali kutokana na mitazamo ya watu kupishana kuhusiana na jambo husika. Kulingana na muktadha huo, msiba wa Steven Kanumba umekumbwa na maneno na hisia kama hizo, hususan mazingira ya kifo chake; kinachosikitisha zaidi watu wengi (ambao wanajitambulisha kama wapenzi wa Kanumba), na baadhi ya vyombo binafsi vya habari vimekuwa vikinihusisha na kifo hicho, kwa kusema kwamba kwa njia moja au nyingine ninahusika na mauaji ya Steven Kanumba. Kwa muda wote huo tangu msiba ulipotokea mpaka leo hii nashika kalamu kujaribu kuyaweka sawa na kuondosha hisia chafu katika fikra za watu, nimekuwa nikipitia katika wakati mgumu sana kwa jinsi ambavyo nimekuwa nikinyooshewa vidole kila upande nikihusishwa na kifo hicho, kiujumla nimezingatia maoni ya wapenzi ya mashabiki wangu wakinitaka kuwa na subira, ila kuna ukweli usemao kwamba, uongo ukirudiwa sana jamii huusadiki na kuuona ukweli, nimeona nisikae kimya ila niweke sawa hili kwamba sihusiki na kifo cha Steven Kanumba.

Nasema wazi kwanza sihusiki kabisa na kifo cha Kanumba kwanza kwa kuzingatia mazingira yenyewe ya kifo kilivyotokea. Wakati kifo hicho kinatokea, nilikuwa sehemu nyingine kabisa na mimi nilikuwa mtu wa tatu kutaarifiwa kwamba Kanumba amepatwa na mkasa ambao baadae ulisababisha kifo chake. Na na hata nilipofika katika hospitali ya Muhimbili (tofauti na watu wanavyodhani kuwa nilifika nyumbani kwake; ukweli mimi nilimkuta tayari amepelekwa Muhimbili), nilikuta tayari alikuwa ameshafariki ndio maana hata Polisi wanaohusika na usalama wa raia, si tu kwamba hawakuniweka chini ya ulinzi, sikuitwa hata kuhojiwa kwa sababu hakuna mazingira yoyote yanayonihusisha mimi na kifo hicho.

Pili, watu wanahusisha tofauti za kibinadamu zilizokuwepo baina yetu na kifo hicho, nasema hii sio sahihi kwa sababu kwanza ni kawaida kwa binadamu kutofautiana, isipokuwa kwetu sisi baadhi ya vyombo vya habari vilikuwa vinakuza kwa sababu nisizozijua, hivyo jamii ikachukulia kuwa tofauti zile ni uadui kitu ambacho sio sahihi, kwani sisi hatukuwa watu pekee tunaotofautiana kwani huu ni mwenendo wa kawaida wa dunia; hivi jana tumeshuhudia Waziri mmoja akieleza bayana katika mkutano na waandishi wa habari kuwa na tofauti na naibu wake, lakini hatuajasikia ikiandikwa wana ‘bifu’ bali imetafutwa lugha nzuri ya kupamba tofauti hizo, kwa kuwa waliohusika ni waheshimiwa, ila kwa wengine kutokana na sababu tusizozijua, inaonekana kama ni haki yetu kuandikwa vibaya. Kinachosikitisha, kwa nini jambo hili linachukuliwa kwa mkazo mkubwa sana, kwani hatujawahi kusikia watu wakiwa wanatofautiana na ndugu jamaa hata na marafiki zao na inaonekana kawaida tu? Kwani vyombo vya habari havikuwahi kuandika kuwa marehemu Steven Kanumba alikuwa na tofauti na baba yake, na yeye mwenyewe alitamka hivyo katika vyombo vya habari, mbona wameliongea bila kuongeza chumvi, na jamii inaona kuwa ni jambo la kawaida la kibinadamu.

Pengine watu wanaojaribu kuongea hayo, hawajui mimi na Steven Kanumba tumetoka wapi? Sisi si watu tuliokutana barabarani, tuna historia katika kazi yetu ya sanaa na pia katika maisha maisha yetu. Mwanzoni kabisa, mimi ndiye niliyempokea Kanumba pale Kaole na ndiye niliyemfundisha sanaa pale (nadhani watu wanakumbuka tamthiliya za wakati huo ITV) na baada ya hapo tulienda pamoja katika kampuni ya Game 1st Quality pamoja na tukafanya filamu kama Johari, Sikitiko Langu, Dangerous Disire na nyinginezo, na tuliendelea kuwa pamoja katika kampuni hiyo mpaka tulipofanya filamu ya Oprah mwaka 2008 ambapo niliingia rasmi kufanya kazi za kampuni yangu, lakini tuliendelea kuwa pamoja hata wakati nikiendelea na kazi za kampuni yangu. Pia mimi nilikuwa wa kwanza kuanza kufanya kazi na Steps na baadae Kanumba alipoanza kufanya kazi zake mwenyewe na kunikuta huko tuliendelea kuwa pamoja kama siku zote. Kitu kikubwa kilichokuwa kinaendelea baina yetu, ni kwamba tulijenga ushindani wa kuendeleza kazi mbele kwa kila mmoja akitoa kazi, mwingine anamjibu, Isitoshe hata vitu vyetu binafsi utaona kama kuna kufanana; kuna wakati Kanumba alinunua Toyota Ruv 4 nyeusi mimi nikanunua ya kijani, aliponunua Harrier na mimi nikanunua pia, na hata gari za hivi karibuni, ukitazama utaona kuwa zinafana kwa karibu; hii ilikuwa ni kama maisha yetu, hatukuwa na uadui, ilikuwa tunapeana changamoto za maendeleo.

Watu wanaojaribu kuonesha kuwa tofauti zetu ilikuwa ni uadui, huwa hawajui wapi tulikotoka ndio maana wanasema wasemavyo na katika kuthibitisha kuwa tofauti hizo hazikufikia katika uadui, kuna watu ambao wanafanya kazi nami katika kampuni yangu ya RJ ndio hao hao Kanumba alikuwa anawatumia siku zote katika kazi zake, hata baada ya tofauti hizo hakuna aliyekoma kufanya kazi na yeyote kati yetu. Hii inathibitisha kuwa tofauti ilikuwa kati yetu kama binadamu, sio chuki za kimafanikio, ingekuwa hivyo watu kama Junior Syaary ambaye mara nyingi hufanya final editing katika RJ ndio huyo huyo alikuwa akifanya na Kanumba, Ally Yakuti ambaye anaandika script za RJ, ndiye huyo huyo aliyekuwa anaandika kwa Kanumba, Steven Shoo ambaye ni mtaalamu wangu wa light, ndiye huyo huyo anayetumiwa na Kanumba na wengine wengi kama Juma Chikoka aliyecheza kikamilifu katika filamu ya kijiji cha Tambua Haki, ambaye pia anashiriki filamu nyingi za RJ, na wote hao, hawakuanzia kwa Kanumba, wote wameanza kwangu mimi ndio niliompatia na hata baada ya hayo yanayosemwa kuwa kuwa ni uadui, sikuwahi kuwakataza kufanya kazi na Kanumba.

Tatu kumtuhumu mtu kwa namna yoyote ile bila ya uthibitisho wa tuhuma hizo, ni kosa kwa sheria za nchi na pia kama ni mfuasi wa dini yoyote ni dhambi, kwani wakati ukisema hayo huku hujui uhalisia bali unasukumwa na nguvu za hisia tu ni sawa na kumchafua mtu huyo katika jamii bila ya kujua jamii inamchukuliaje. Napenda kusema wazi wazi kuwa, kwa kila anayetekwa na wimbi hili, ajaribu kufikiria leo ipo kwangu mimi, kesho inaweza kuhamia kwako, kwani mimi sio wa kwanza kufikwa na haya, inaweza kukukuta hata wewe au ndugu yako, utajisikiaje. Na kama kweli mimi nimehusika na kifo cha Kanumba kwa namna yoyote ile, basi Mungu atanihukumu na kila aliye hai atashuhudia, ila kama sijahusika kwa lolote, Mungu hatonihukumu na badala yake ataniinua, kwa kuwa ninapita katika kipindi kigumu mno sasa hivi kwa madhila haya.

Mwisho kabisa napenda kumaliza kwa msemo usemao, ajidhaniaye amesimama, aangalie asianguke, kwani kadri mambo haya yanavyoendelea, usidhani yataishia kwangu, kwani mkono wa dhuluma haushii karibu, ukisikia jirani anapiga kelele za mwizi, usilale kamsaidie, usiseme kuwa hatuhusiki kwani hayupo kwetu, kesho utafikwa na wewe utakosa wa kukusaidia. cha msingi kama tunampenda sana ndugu yetu ni kumuombea kwa Mungu, kwani hatujui makao yake huko aliko, na sio kuunda vitu ambavyo kamwe hata yeye angekuwa hai asingeviafiki.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU STEVEN KANUMBA MAHALI PEMA
PEPONI
MUNGU IBARIKI AFRIKA MUNGU IBARIKI TANZANIA

Thursday, April 12, 2012

MCHEZA FILAMU TANZANIA, VINCENT KIGOSI (RAY) THE GREATEST AMPA POLE MAMA WA MAREHEMU STEVEN KANUMBA (THE GREAT) NA KUONYESHA JINSI ALIVYOJISHUGHULISHA KATIKA SUALA LA KUMUWEKA MAHALI PA KUPUMZIKA MILELE RAFIKI YAKE
 Muda ulifika wa Mama Kanumba kuwasili uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere maana wakati mauti yanamfika mwanae alikuwa safarini Bukoba.Mama yangu mzazi(mwenye nguo nyeupe) ndiye aliyeongoza msafara wa kwenda kumpokea Mama Kanumba

 Kamati ya mapokezi ikimsubiri Mama Kanumba kuwasili.

 Muda ulifika na Mama akawasili na majonzi yakatawala.

Kilio na simanzi vilitawala uwanjani hapo(kulia) ndiye Mama yangu mzazi, Mama Mary Kigosi akimsaidia rafiki yake.

 Pole sana Mama kwa msiba mkubwa uliokupata ninakuwaidi nitakuwa pamoja nawe kwenye shida na raha

Mama alishindwa kabisa kuzuia hisia zake mpaka kuzimia.
 Njiani kuelekea msibani.

 Tukimsubiri Mama mzazi wa Marehemu Kanumba.

Baada ya kufika nikaenda kumpa pole,alilia sana aliponiona na kuniambia pacha wako mwanangu yuko wapi umebaki peke yako? Niliumia sana.

 Mazungumzo yakaendelea.

Akia kwa uchungu mkubwa sana. Pole mama.

 Kesho yake nikaenda kutafuta jeneza la kumzikia ndugu yetu mpendwa.

Hili ndilo jeneza aliozikiwa Marehemu Steven Kanumba.

 Baada ya kutoka kwenye majeneza nikaenda kuwachukua maskali kwa ajili ya postmortem

 Tukiendelea kusubiria.

Nikiwa nimeshamaliza hatua zote.

Tuesday, April 10, 2012

STEVEN KANUMBA AANDIKA HISTORIA NYINGINE BAADA YA BABA WA TAIFA

Watanzania hii leo wameweza kumuaga kwa heshima mwigizaji nyota marehemu Steven Kanumba katika ibada iliyofanyika kwenye viwanja vya Leaders club Kinondoni jijini Dar es salaam,na kuhudhuriwa na Makamu waRais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania mh.Dkt Gharib Bilal,mke wa Rais mama Salma Kikwete na viongozi wengine pamoja na familia ya marehemu,waigizaji wenzake pamoja na wanakwaya wa kwaya ya Neema gospel (NGC)kutoka AIC Chang'ombe alikokuwa muumini na mwanakwaya wa kwaya hiyo.

Umati mkubwa ambao ulikusanyika katika eneo la Leaders club kisha makaburi ya Kinondoni umeweka historia kwajinsi msanii huyo alivyokubalika katika jamii ya Watanzania,mpaka sasa akiwa ameshika nafasi ya pili kupata watu wengi,nafasi ya kwanza ikiwa ni msiba wa Baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye mwili wake ulitolewa heshima za mwisho kwenye uwanja wa zamani wa Taifa jijini Dar es salaam.
Sehemu ambayo ilikuwa ikiandaliwa kuwekwa jeneza lenye mwili wa Kanumba.

Hemed pamoja na Yusuph ambao ni waigizaji wakiingia Leaders asubuhi ya leo kumuaga mwenzao.

Watoto ambao waliigiza na Kanumba wakiwa wanaingia viwanjani hapo asubuhi ya leo.

Mama wa marehemu Steven Kanumba akiwapungia maelfu ya watu asubuhi ya leo kuonyesha shukrani kwa kujitokeza kumuaga mwanae.


Viongozi wa serikali wakiwa wamekaa kwenye jukwaa maalumu.


Kijana Samuel Limbu akiwaongoza wenzake wa Neema gospel Choir kuimba viwanja vya Leaders club.

Wasanii wakiliingiza jeneza la mwenzao viwanja vya Leaders Kinondoni.

Wasanii wakipeleka jukwaani jeneza lenye mwili wa Steven Kanumba.

Waigizaji wakishusha jeneza la mwenzao taratibu jukwaani.

Jukwaa kuu kwaya ya Neema Gospel Chang'ombe wakiimba kumsindikiza mwimbaji mwenzao.


Kuna watu walishindwa kuhimili hisia zao kwa marehemu nakujikuta wakizimia,msalaba mwekundu wakitoa huduma.

Makamu wa Rais Dkt.Gharib Bilal akitoa heshima zake za mwisho.

Mke wa Rais mama Salma Kikwete akitoa heshima zake za mwisho.


Baadhi ya umati wa watu uliokuwepo asubuhi ya leo viwanja vya Leaders club Kinondoni.

Mh.Bernard Membe akitoa heshima zake za mwisho.

Kamanda wa polis mkoa wa Dar es salaam Kova akitoa heshima zake za mwisho.

Wanahabari wakihakikisha hawapitwi na jambo.
KUTOKA MAKABURI YA KINONDONI NAKO HUKO MAELFU YA WATU WALIKUSANYIKA ILI KUSHUHUDIA MAZISHI YAKE,AMBAPO POLISI WALIKUWA NA KAZI YA ZIADA KATIKA ULINZI,AMBAPO PIA TAARIFA ZINASEMA KUNA WATU WAMEJERUHIWA BAADA YA KUANGUKA KUFUATIA TAWI WALILOKALIA KUKATIKA.